Kutoka Katika Mkusanyiko
wa Risala za Nuru
NENO LA
ISHIRINI NA SITA
SAID NURSI
Kutoka
Katika Mkusanyiko
wa
Risala za Nuru
Suwahili
Lisanýna Tercümesi
Kadari ya
Kiungu na Hiari ya Mwanadamu Kwa Muujibu wa Madhehebu ya Kiislamu ya Ahl al-Sunna wa'l-Jama'ah
“15:21 Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; Wala
hatukiteremshi chochote ila kwa kipimomaalum (kilichokwisha kuamuliwa - si
hovyo hovyo tu).
(Wa im-min shay-in illaa 'indanaa khazaainuhuw, wamaa nunazziluhuw illaa
biqadarim - ma'aluwm).”
“36:12 .. Na kila kitu Tumekihifadhi katika Daftari Linalobainisha
(kila kitu). (Wa kulla
shay-inahswaynaahuw fiy Imamim-Mubiyn).”
[Kadari na hiari ya mwanadamu ni
mawazo mawili yanayohusiana ambayo tumekusudia kuyaeleza katika Maudhui Manne.]
Maudhui ya
Kwanza
Kadari na hiari yamwanadamu,
ambavyo huashiria viwango vya juu kuliko vyote vya ukamilifu wa imani ya mtu na
utii, ni kitu kinachohusiana na uzoefu wa kindani na hali ya kiroho ya muumini;
kwa hivyo sio kitu kinachothibitishwa kwa sayansi au nadharia. Mwanadamu anayo
hiari, na ameamriwa kufuata wajibu wa kidini. Kwa vyovyote vile mtu hawezi
kusingizia dhambi zake kwa Allah. Kadari ya Kiunguipo ili imzuie
mwanadamuasijivuniematendo yake mema kwa kuyasingizia kwake yeye mwenyewe. Mwanadamu
anayo hiari ili roho asi yenye matamanio ya kimwili isijivue matokeo ya dhambi
zake kwa kuisingizia Kadari, wakati mtu mcha-Mungu anaweza kusingizia mema yake
yote kwake yeye mwenyewe peke yake.
Inaweza kuruhusiwa
watukuyahusisha matukio ya zamani na ya mikosi na Kadari ya Kiungu, ili mtu
asikatike tamaa anapokumbwa na maafa, ingawa hakuna mtu anayesamehewa dhambi
zake na kukwepa wajibu wake kwa kusingizia Kadari kila kitu. Kwa hivyo, kuamini
Kadari kumejumuishwa miongoni mwa nguzo za imani ili kumhifadhi mwanadamu asiwe
na kiburi, na hiari ya mwanadamu inatambuliwa kuwa ndio msingi wa dhambi zake.
Mwanadamu anawajibika mia kwa mia
kwa dhambi zake kwa sababu ni yeye mwenyewe ambaye ndiye huamua kuzitenda,
kisha ndipo hufanya hivyo.Dhambi ni chanzo cha vurugu na uharibifu mwingi, kwa
hiyo zinaweza kustahili adhabu kali - kwa kutoa mfano, nyumba inaweza kuunguzwa
mpaka ardhini kwa kuwasha kibiriti tu..Kwa upande mwingine, mwanadamu hana haki
ya kujigamba kuhusu matendo yake mema kwa kuwa, kwa hakika, anao mchango mdogo
sana juu yake. Ni Huruma ya Kiungu ambayo inakutarajiautende mema, na ni Uweza
wa Mola ndio unaoyaunda. Allah humwongoza mwanadamu kwenye matendo mema, na
humfanya afaulu kuamua na kuyatenda . Kwa hivyo chanzo cha matendo mema ya
mwanadamu ni Takwa la Kiungu. Mwanadamu anaweza kuwa nayo hayo kwa njia ya
kuamini na kuombakwa Allah ili uweze kustahili kuwa nayo, huku akiamini kwa
dhatiumuhimu wa kuyatenda na kufurahia yale ambayo Allah Amemuamuru kwa ajili
yake. Ni mwanadamu mwenyewe, kwa upande mwingine, ambaye husababisha dhambiama
kwa njia ya uwezo na uamuzi au kwa njia ya kuchagua na kupendelea, kama vile
ambavyo mwanga mkali wa jua unaweza kusababishavitu vinavyoweza kuoza
viharibike na kuvunda.
Mwanadamu huamua na hutenda
dhambi, lakini ni Allah Anayeumba matendo yake yote yawe mazuri au mabaya.
Allah huumba tendo la dhambi kwa nia njema. Ingawa mwanadamu hupata faida
nyingi inyeshapo mvua, mtu ambaye kapata dhara fulani iliyosababishwa na mvua
hiyo hawezi kusema kuwa mvua haina huruma yeyote ya Allah kwa ajili ya
mwanadamu. Ni kwa sababu ya ukweli huu uliofichika basikuamua na kutenda dhambi ni uovu, lakini uumbaji wa hayo matendo sio
uovu. Kuumba ni kuzuri kabisa, kwa asili yake wenyewe, kwa kuwa daima hutoa
matokeo mazuri. Kwa hivyo ubaya katika matendo ya mtu hutokana na kuamua na uwezo, na wala
hautokani naTakwa la na Uumbaji wa Kiungu .
Kwa kuwa Kadari ya Kiungu haina
uovu au ubaya wowote kuhusiana na matokeo, pia haina maonezi kwa sababu ya
vyanzo. Kadari ya Kiungu kila mara hutia maanani chanzo cha kwanza, siyo vyanzo
bandia vya pili, na daima hutenda haki.
Kwa upande mwingine, wanadamu
huhukumu kwa muujibu wa vyanzo bandia na Hufikia uamuzi potofu. Kwa
mfano,mahakama inaweza kumfunga mtu kwa kosa la wizi na kumuonea kwa sababu
hajatenda kosa la aina hiyo; lakini Kadari ya Uungu hutoa hukumu ya aina hiyo
kwa sababu ya mauaji ambayo huyo mtu katenda lakini imebakia siri asiyoijua
mtu. Kwa hiyo, wakati mahakama imemuonea mtu huyo kwa kumlaumu kwa kosa ambalo
hakulitenda, Kadari ya Kiungu imemuadhibu kwa kosa ambalo halikujulikana. Funzo
la mfano huu ni kwamba Allah hutenda haki thabiti katika kila jambo, ambapo
mwanadamu anaweza asitende haki. Kadari ya na Uumbaji wa Kiungu umetakasika
kabisa na uovu na ubaya hapo mwanzo na hata mwisho wa matendo yenyewe, na kwa
ajili ya chanzo na matokeo.
Suali: Iwapo mwanadamu anao
mchango mdogo sana katika matendo yake kwa sababu hiari yake haina uwezo wa
kiundaji, kwa nini tunasoma katika Qur'an kwamba Muumbaji wa Mbingu na Ardhi
Anauchukia hivyo uasi wa mwanadamu?
Jibu: Kutokuamini, uasi, na
udhambi vinamaanisha uharibifu, na uharibifu kamili unaweza kutokana na tendo
la kutotii lenye uzito mdogo kabisa. Kama vile chombo kinavyoweza kuzama kwa
sababu ya uzembe wa nahodha, wakati juhudi za mabaharia wote zinashindwa
kukiokoa. Hiari ya mwanadamu huweza kusababisha uharibifu mkubwa, kutokana na
kutoamini na udhambi, hata kama mchango wake katika kutenda matendo ni mdogo
mno. Kutoamini ni dhambi kubwa mno kwa asili yake kiasi kwamba huushusha
ulimwengu mzima uwe hauna thamani, na kunapinga ushahidiliaji wa Upweke wa
Allah wa viumbe wote, na kunakanusha udhihirishaji wa Majina ya Kiungu. Kwa
hivyo ni sawa kabisa kwa Allah kukuchukulia kutoamini kuwa ni kosa kubwa sana
na kuwatishia wasioamini kwa ukali sana kwa jina la viumbe wote na Majina ya
Kiungu, na ni haki kabisa kuwahukumu waingie Motoni kwenye mateso ya milele.
Kwa kuwa watu waasi husababisha ufisadi mkubwa sana kwa njia ya kutoamini na
udhambi , waumini wanahitaji sana msaada wa Allah dhidi yao.Mvulana mtukutu
anaweza kuiteketeza nyumba nzima kwa moto ingawa inalindwa na wanamume kumi
wakubwa, na hao walinzi wanahitaji kuomba kwa baba wa huyo mvulana ili kumzuia
asitende kosa hilo la jinai. Halikadhalika waumini wanahitaji msaada wa Allah dhidi ya
watu waasi na wadhambi.
Kwa ufupi: Inaruhusiwa muumini
kuongelea Kadari ya Kiungu na hiari ya mwanadamu pindi imani yake ni kamilifu
na pindi awapo kakomaa ya kutoshakutambua kuwa viumbe wote pamoja na yeye
mwenyewe wapo chini ya Allah. Anatekeleza wajibu wake kwa sababu ana hiari na
anamtukuza Allah kwa kumtangaza kuwa hahusiki kabisa na madhambi yake. Kamwe
hasau kuwa yeye ni mtumishi wa Allah, na hivyo anajaribu kufuata Amri zote za
Kiungu. Kwa upande mwingine, anabakia mwenye shukurani nyingi kwa Allah kwa kuisifu
Kadari ya Uungu kwa kumuwezesha atende kila jema aliloweza kulitenda, na kamwe
yeye hajivunii hayo. Pia anapata nguvu za kuvumilia mikosi yake yote kwa
kutambua kuwa ndani yake mna Kadari.
Hata hivyo, sio sawa kwa yeyote
anayepuuza Amri za Kiungu kubishia habari za Kadari ya Kiungu na hiari ya
mwanadamu, kwa sababu fikra zake potofu zitamfanya asingizie vyanzo kwa uumbaji
wote na ampuuze kabisa Allah. Huteka nyara ufundi na matendo yake mema, na
kuyahesabu kuwa haya yote yametokana na yeye mwenyewe, na husingizia Kadari
makosa yake yote na kushindwa kwake kote. Oni hili ni sawa na kurahisisha
Kadari ya Kiungu na hiari kuwa ni mtego wa kipuuzi anaotegewa mwanadamu na
nafsi yake mwenyewe (nafs ammara) ili
kumpotosha hadi apuuze na akanushe wajibu wake wa kidini.
Maudhui ya
Pili
Somo hili ni gumu sana na limekuw
likiwatatiza wanazuoni kwa muda Mrefu, hivyo linaweza kueleweka kwa watu wenye
ufahamu wa ndani Na ujuzi mkubwa. Kadari ya Kiungu na hiari ya mwanadamu
Vinaweza kupatanishwa kwa njia saba.
Njia ya
Kwanza:
Mpangilio kamili na ulinganifu unaoonyeshwa na na viumbe vyote vinashuhudia
kuwa Allah ni Mwenye Hekima Zote na Haki. Hekima na Haki vinahitaji mwanadamu
awe na na hiari ili aweze kuadhibiwaau kuzawadiwa kwa matendo yake. Ingawa
hatuwezi kujua hali halisi ya hiari hiyo, na huenda tutashindwa kuipatanisha
uzuri na Kadari ya Kiungu, hiyo haimaanishi kuwa hiari haipo.
Njia ya
Pili: Kila
mtu huhisi anayo hiari, na huiona kuwa ipo. Kujua asili ya kitu ni tofauti na
kujua kuwa kipo. Kuna vitu vingi ambavyo kuwepo kwake tunakujua wazi, wakati
asili yao haieleweki. Hiari ya mwanadamu ni moja ya vitu hivyo, na kuwepo kwake
hakutegemei idadi ya vitu tunavyovijua; kwa hivyo, kutokujua kwetu kwa kitu
fulani hakuna maana kuwa hakipo.
Njia ya
Tatu:
Hiari ya mwanadamu haipingani na Kadari ya Kiungu, bali, Kadari ina thibitisha
kuwepo kwa hiari. Kadari ya Kiungu kwa namna fulani ni sawa naUjuzi wa Kiungu,
ambao unakwenda sambamba na hiari ya mwanadamu, katika kuamua matendo yake. Kwa
hivyo 0unaithibitisha Kadari, na hauikanushi.
Njia ya
Nne: Kadari
ya Kiungu ni aina ya ujuzi, na ujuzi hutegemea kitu ambacho unakijua. Yaani
ujuzi wa wazo fulani sio muhimu katika Kujua kuwepo kwa kitu kinachojulikana.
Kinachojulikana, katika kuwepo kwake kwake nje, hutegemea Pawa ya Kiungu
inayofanya kazi kupitia kwa Takwa la Kiungu.
Pia, milele ya zamani, sio kama wanavyodhani wengi, ni pahala pa kuanzia
“wakati” ili iwe muhimu kwa kuwepo kwa vitu. Milele ya zamani, kwa kweli ni
kama kiyoo ambamo wakati wote - wa zamani, wa sasa, na wa baadae, unaonekana.
Katika kujiondosha katika uendeleaji wa wakati, watu wana tabia ya kudhani kuwa
mwisho wa wakati wa zamani ni mlolongo wa vitu fulani wanaouita “azel” -milele iliyopita. Lakini kuhoji
kwa muujibu wa dhana kama hiyo sio sahihi wala haikubaliki. Mfano ufuatao
utasaidia kuielewa hoja hii uzuri:
Jifikirie kuwa wewe umesimama na
kiyoo mkononi mwako, na kuwa kila kinachoonekana upande wa kuliamle
kinawakilisha ya zamani, na kila kinachoonekana upande wa kushoto mle
kinawakilisha ya baadae.
Kiyoo kinaweza kuonyesha sura ya
upande mmoja tu, kwa kuwa hakiwezi kuonyesha sura zote mbili kwa wakati mmoja
ule unapokishika hicho kiyoo.
Ukiwa unataka kionyeshe sura zote
mbili kwa wakati mmoja, itakubidi upande juu ya pahala ulipokuwepo mwanzo, ili upande
wa kulia na kushoto viungane kuwa kitu kimoja, na hakuna kinacobakia kuitwa cha
kwanza au cha mwisho, mwanzo au mwisho. Kama ilivyokwisha kutajwa, Kadari ya
Kiungu kwa njia fulani ni sawa na Ujuzi wa Kiungu. Inaelezewa katika usemi wa
kinabii hivi:
“Yenye nyakati zote na matukio yote katika nukta moja. Ambako ya kwanza
na ya mwsiho, mwanzo na mwisho, kilichotokea na kitakachotokea, vyote
vimeungana kuwa kitu kimoja”.
Nasi hatukuwachwa mle ili
uelewaji wetu wa wakati na matukio uwe kama kiyoo cha nafasi ya zamani.
Njia ya
Tano:
“Chanzo na athari” havitofautiani kwa muujibu wa Kadari, yaani imekusudiwa kuwa
hiki “chanzo” kitazaa “athari” ile. Kwa hivyo haiwezi kusemwa, kwa mfano kuwa, “kumuua mtu kumpiga risasi” kusihesabiwe
kuwa ni kosa la jinai kwa sababu tu huyo aliyeuliwa alikusudiwa kwa vyovyote
vile afe wakati ule; na kwa hivyo angekufa tu hata asingepigwa zile risasi.
Hoja kama hiyo haina msingi kwa vile mtu yule amekusudiwa atakufa kwa kupigwa risasi. Hoja isemayo kuwa
angelikufa hata kama asingepigwa risasi ingemaanisha kuwa alikufa bila chanzo,
na kwa hiyo tusingeweza kueleza jinsi alivyokufa. Sharti ikumbukwe kuwa hakuna aina mbili za kadari – moja kwa
ajili ya chanzo, na nyingine kwa ajili ya athari. Kadari ni moja tu.. Baada ya kughilibiwa na kweli iliyo kama uongo
ya aina hii, dhehebu la Mu'utazili (the Mu'utazili
school of thought) likafikia uamuzi kuwa: “yule mtu asingelikufa kama
hangepigwa risasi” (wanasahau kuwa ilikuwa kadari yake kupigwa risasi), wakati
dhehebu la Mujabbira (the Mujabbira
school of thought = Fatalists) likasema kuwa “mtu yule angekufa hata kama
asingalipigwa risasi”.Dhehebu la Ahl
al-Sunna wa'l-Jama'a hufuata msimamo sahihi kuamuakwamba, “Hatujui kama
angalikufa au asingelikufa kama asingalipigwa risasi”.
Njia ya
Sita: Wafuasi
wa Imam al-Maturidi, moja ya tawi la dhehebu la Ahl al-Sunna wa'l-Jama'ah,
maelekeo ya mwanadamu ambayo hutegemea hiyo hiari yake, ina thamani ndogo na
kuwepo kudogo tu. Lakini dhehebu la Ash'arite linasema kuwa yale maelekeo
hayamtegemei mwanadamu kwa sababu linahesabu kuwa.Kwa muujibu wao, mwanadamu
hata hivyo anao uwezo mdogo au wa kinadharia tu wa kuyatumia hayo maelekeo; na
kwa sababu hiyo, maelekeo na matumizi yake ni mambo ya kulingana, wala hayapo
kihalisi.Kitu chenye kuwako kidogo na ya mlingano, hakihitaji chanzo kikamilifu
na stadi ambayo itabatilisha hiari ya mwanadamu katika matendo yake. Lakini iwapo chanzo chake
kinakuwa na, basi kitakuwa na kuwepo halisi. Kwa hivyom pale Qur'an inaposema:
“Usifanye hiki, kwa kuwa ni kiovu”, anaweza kujizuia asikifanye.
Mwanadamu angalikuwa ni muundaji wa matendo
yake yeye mwenyewe, basi angekuwa yeye mwenyewe ndiye chanzo cha matendo yake,
na hiari yake ingebatilika. Kwa kuwa, kwa muujibu wa sayansi ya misingi
iliyosimikwa na mantiki, ikiwa kitu sio
muhimu basi hakitokuwepo. Maana ya hii ni kwamba, sharti kiwepo chanzo
Halisi kamili kabla kitu hajakuwepo; lakini chanzo kamili hufanya kuwepo kwa
kitu muhimu, hivyo patakuwa hakusa nafasi ya uchaguzi.
Suali: Matendo ya mwanadamu ni
matokeo ya upendeleo wake baina ya chaguzi mbili, ambayo yana maana ndogo sana.
Iwapo chanzo muhimu hakipo ambayo inamlazimisha afanye upendeleo, basi hii
inamaanisha kuwa hilo tendo la kupendelea linatokea bilachanzo muhimu. Si
mantiki isiyowezekanaambayo huupinga mmoja wa misingi muhimu ya thiolojia?
Jibu: Sio jambo lisilowezekana kuwa
mtu hufanya upendeleo bila chanzo muhimu, ni tabia ya hiari yake hiyo kufanya
mambo namna hiyo. Hata hivyo ni jambo lisilowezekana kuwa jambo linaweza
kupendelewa peke yake bila chanzo muhimu cha upendeleo wake.
Suala: Kwa kuwa ni Allah Ndiye
Anayeumba tendola mauaji, kwa nini basi mtu anayeua anaitwa muuaji?
Jibu: Mwanadamu huamua kufanya jambo
na kisha hulifanya; kwa hivyo yeye Ni mtendaji au wakala wa matendo yake. Ni
mtu mwenyewe anayefanya tendo la kuua; kwa hivyo lazima aitwe muuaji. Allah
huumba matendo ya mwanadamu kwa vile huyapa hali ya kuwepo. Allah hayatendi
matendo yale. Isingekuwa na maana iwapo mwanadamu kuwa na hiari iwapo Allah
hajaumba matendo yenyewe ambayo ni matokeo ya ileh hiari.
Njia ya Saba
Ingawa hiari ya mwanadamu ni dhaifu mno
kusababisha jambo litokee, Mwenye Enzi Kuu Allah, Mwenye Hekima isiyo kiwango,
kaufanya utekelezaji wake uwe ni sharti jepesi la kutekelezeka Takwa Lake la
kimataifa. Humwongoza mwanadamu kuelekea kokote ambako mwanadamu anakotaka kwa
njia ya hiari yake, ili abakie anawajibika kwa matokeo ya uchaguzi wake. Kwa
mfano, ukimchukua mtoto mabegani mwako, kisha umwache huru aamue anakotaka
kwenda na akakuchagulia umpeleke katika mlima mrefu, na akatokezea kupata
mafua, hatakuwa na haki ya kukulaumu wewe kwa hilo. Naam huenda hata utamuadhibu kwa
sababu alipenda kwenda mlimani. Halikadhalika, Mwenye Enzi Kuu Allah, Hakimu wa
Haki kuliko
Mahakimu wote, kamwe hamshawishi
mja Wakekufanya jambo lolote, na Ameumba Takwa Lake kwa kutegemea kwa namna
fulani hiari yamwanadamu.
Kwa ujumla:
Ukiwa
wewe ni mtu, basi unayo hiari, ambayo haina mchango wowote wa maana kwenye
matendo yako mema, inagawa inaweza kusababisha dhambi na uharibifu wa hatari
sana popote itakapotumika. Kwa hiyo itumie hiari yako kwa faida yako
mwenyewekwa kumuomba Allah nyakati zote, ili ufaidi baraka za Peponi, tunda la
mlolongo wa matendo mema, na uifikie furaha ya milele. Tena sharti kila mara
umuombe msamaha Allah kwa dhambi zako, ili ujizuie na kutenda matendo maovu na
uokolewe na mateso ya Motoni, tunda la mlolongo uliolaaniwa wa matendo maovu.
Sala na kuiweka imani yako kwa Allah huimarisha sana maelekeo (inclination)
kutenda mema, na kutubia na kuomba msamaha wa Allah huyakatilia mbali maelekeo ya
kutenda maovu na huvunja mahalifu yake.
Maudhui ya
Tatu
Kuamini Kadari ya Kiungu ni moja
ya Nguzo za Iman, na kwa muujibu wa imani hii, kila kitu ulimwenguni
hutamalikiwa na Allah, Mwenye Nguvu Zote. Wakati kukiwa na ushahidi mwingi
usiohesabika wa Kadari, inaweza kutosha hapa kutoa maelezo ya utangulizi
kuonyesha jinsi Nguzo Hii ilivyo muhimu kwa viumbe wote.
Qur'an inaeleza waziwazi kuwa
kila kitu hupangwa kabla, kisha ndipo kinarikodiwa baada ya kutokea, kama aya
nyingi pamoja na hizi zifuatazo zinavyoonyesha:
“6:59.. (Hapana chochote) kilichorutubika walakilichoyabisika, ila
kimo katika Kitabu kidhihirishacho kila jambo. (Wa laa rutwbin wa laa yaabisin illaa fiy Kitaabim-Mubiyn)”
Usemi huu wa Qur'an
umethibitishwa na ulimwengu, hii Qur'an-kubwa ya Uweza wa Kiungu, kwa njia zake
za ishara za uumbaji na za utekelezaji kama mpangilio, ulinganifu, mizania,
kuunda na kutia sura, kupamba na kubainisha. Mbegu zote, kokwa za matunda, uwiano
uliopimwana maumbile – vyote vinaonyesha kuwa kila kitu kimepangwa kabla kabla
hakijawepo duniani. Kila mbegu au kokwa ya ttunda ina gamba lindaji lililoumbwa
kwenye karkana ya Kaf Nun, ambamo
Kadari ya Kiungu imejengea humo historia nzima ya maisha ya mmea au mti wake:
“Qur'an inasema kuwaAmri Yake Pindi Atakapo kuumba kitu kiwepo ni kukiambi, Kuwa, nacho
huwapo. Tafsiri ya mwanzo ya Kiingereza “Kuwa na ikawa” ni “KUN FA
YAKUWN”. Katika mapokeo ya Kiislamu, uumbaji wote unahesabika kutokana na
Amri ya Kiungu. KUN! Hii KAF yaani
-k- na NUN yaani -n- ni herufi mbili zinazounda neno KUN ambalo maana yake ni Kuwa!”
Uweza wa Kiungu hutumia punjepunje kwa muujibu
wa kipimo kilichowekwa na Kadari ya Kiungu, ili kuifanya kokwa ile kuota
kimiujiza iwe mti maalum. Hii Maana yakeni kwamba historia ya baadae ya maisha
ya mti ule inakuwa kama vile Imeandikwa ndani ya mbegu yake.
Ingawa zipo tofauti baina ya kila kiumbe, na
baina ya kilakabila (species), malighafi ya msingi inayoumbiwa wanyama na miti
ni sawa. Mimea na wanyama vinavyoota kutoka katika elementiza msingi sawa
huonyesha, juu ya utofauti wao, ulinganifu na uwiano kiasi kwamba mwanadamu
hulazimika kutambua kuwa kila mmoja wao kapewa umbo na kipimo chake maalum.
Ni Uweza wa Kiungu ndio unaompa kila mmoja umbo
kulingana na kipimo kilichowekwa yake na Kadari ya Kiungu.kwa ajili yake. Kwa
mfano, hebu fikiria jinsi idadi kubwa sana ya punjepunje zisizokuwa hai
zinavyohama, zinaungamana, zinatengana, ili mbegu hii ikue iwe mti huu au tone
lile la shahawa likue liwe mnyama yule.
Kwa kuwa yapo madhihirisho ya Kadari ya Kiungu
kiasi hiki katika vitu vinavyoonekana, kwa hakika,maumbile ambayo huvivika vitu
kadiri muda Unavyopita, na hali vinavyoipata kwa njia ya miendo yao, pia
hayategemei amri za Kadari ya Kiungu. Naam mbegu moja huonyesha Kadari kwa njia
mbili, moja kwa Kukionyesha Kitabu kidhihirishacho kila jambo (Kitabu
Dhihirishi = Kitaabum - Mubiyn ),
ambali ni jina jingine tu la Takwa la Kiungu, na sharia za kiumbaji na
kiutendaji za ulimwengu. Njia nyingine ni kwa kuonyesha Rikodi Dhihirishi (Imaamum-Mubiyn), ambalo ni jina lingine
la Ujuzi na Amri ya Kiungu and Command).Tukiyahesabu haya mawili kuwa ni
madhihirisho tofauti ya Kadari ya Kiungu, hiyo ya kwanza inaweza kuelewekana
kuitwa “Kadari Halisi”, na hiyo ya pili iitwe “Kadari Rasmi au ya Kinadharia”. Umbo la baadae la mti
uliokwishakukua linaweza kueleweka kuwa ni Kadari Halisi yake, wakati Kadari
Rasmi ni pamoja na awamu zote ambazo huo mti Sharti upitie katika maisha yake,
na kuelewa historia nzima ya maisha yake. Udhihirisho kama huo wa Kadari ya
Kiungu, ambao unaonekana kwa urahisi hivyo katika maisha kama yale ya mti,
huonyesha jinsikila kitu kilivyopangwa kabla katika Rekodi kabla ya kuja kwake
duniani. Kwa upande mwingine, matunda yote na mbegu na mbegu zote ambavyo ni
ishara ya Kitabu Dhihirishi (Kitabum-Mubiyn)
na Rikodi Dhihirishi (Imamum-Mubiyn),
panmoja na kumbukumbu (memories) zote za mwanadamu ambazo zinaashiria Ubao
Hifadhishi (Lawhum-Mahfuwdhw),
wadhihirisha kuwa, kwa kuwa kila kitu kilirikodiwa kabla, historia ya maisha
yake pia imerikodiwa. Historia ya maisha ya kila mti, kwa mfano, imerikodiwa
katika kila tunda lake, ambao ni matokeo ya maisha yake yote. Historia ya
maisha ya mwanadamu pamoja na matukio yanayotokea katika dunia ya nje yote
yamerikodiwa katika kumbukumbu yake. Kwa hivyo Pawa ya Kiungu huandika matendo
ya mwanadamu yule kwa Kalamu ya Kadari kwa kuitia katika kumbukumbu yake ili
aweze kuja kuikumbuka Siku ya Hesabu Mwanadamu sharti ahakikishiwe kuwa katika
dunia hii ya mpito na misukosuko kuna “viyoo” vingi vinavyohusu umileleambavyo
kwavyo Mwenyewe Mwingi wa Pawa na Hekima huonyesha na hudumisha ujulikano wa
viumbe ambavyo hufa. Pia kuna mbao nyingi ambazo Mhifadhishi Mwenye Ujuzi Wote
huandika maana za viumbe vya mpito.
Kwa ufupi: Wakati mimea, ambayo
ndio daraja la chini zaidi kuliko yote la maisha, hutegemea mia kwa mia Kadari
ya Kiungu, inadhihirika pia kuwa maisha ya mwanadamu, ambaye ndio daraja la juu
zaidi kuliko yote, hutegemea kidogo sana hiyo Kadari. Kama ambavyo matone ya
mvua ni ishara ya wingu, na mmiminiko wa maji unadhihirisha chemchemi, na
stakabadhi na vocha huashiria kuwepo kwa leja, vivyo hivyo ndivyo matunda,
mbegu zake, shahawa, na maumbo huashiria Kitabu Dhihirishi na Rikodi
Dhihirishi.
Maneno haya “Kitabu Dhihirishi” huashiria Kadari Halisi, ambalo ni jina laTakwa
la Kiungu na sheria za Allah za kiumbaji na kiutendaji za ulimwengu, na
mpangilio wa kiummbileunaoonyeshwa na viumbe hai. Rikodi Dhihirishi inamaanisha
Ubao Hifadhishi ambao ndio Kitabu cha Ujuzi wa Kiungu na unaashiria Kadari
Halisi au ya Kinadharia inayoweka mpangilio wa vitu visivyokuwa na umbile na
maisha ya ulimwengu.
Kwa kumalizia: Tunashuhudia kuwa katika
wakati wotewa ukuaji, wa viumbe hai punje huwa na mwendo wa kudumu na husafiri
kwenda ziendako kupitia njia tata na hubakia kule. Mwendo wao huo huzaa faida, matumizi,
na mifano ya busara. Bila shaka Kadari ya Kiungu hukipangia kila kitu kipimo
fulani. Ikiwa hivi ndivyo, yaonekana pia kuwa hata hali zisizokuwa na umbo za
viumbe hai huzaa matunda fulani. Kwa hivyo Pawa ya Kiungu ni wakala na Kadari
ya Kiungu ni mtindo. Tunaona kuwa kila mwendo kinaokwenda kiumbe chochote
katika maisha yake yote,na hatua zote ambazo kiumbe hicho kinazipitia
zinapangwa kabla na Kadari ya Kiungu na maisha yake yote yanaunda umoja
linganifu.
Kwa kuwa tunaelewa kuwaKadari ya
Kiungu imekipangia kila kitu muishio na matokeo fulani yenye malengo, na kwa
hivyo hatua zote katika maisha yake zimepangwa kabla na hiyo hiyo Kadari, bila
shaka historia ya maisha ya mwanadamu, tunda kamilifu zaidi kuliko matunda yote
ya mti wa uumbaji, khalifa wa Allah hapa ardhini, na mchukuaji imani Yake kubwa
zaidi kuliko zote, anawajibika zaidi na sheria ya Kadari ya Kiungu.
Suali: Ikiwa sote tumefungwa
kiasi hicho na Kadari ya Kiungu, basi kuamini hivyo hakuleti mushkili na
wasiwasi kwa roho inayopenda utendaji kazi wa bila kusitisha na kujifanya
mkamilifu?
Jibu: Hakuleti mushkili, bali
huipa roho afuweni, usalama, na starehe. Endapo Mwanadamu haiamini Kadari, basi
roho yake italazimu ibebe mzigo mzito kama dunia kwa ajili ya uhuru wa muda
mfupi, kama wa kuota tu, na kwa kweli ni kidogo (limited) sana. Mwanadamu
kaungana na ulimwengu wote, wakati anayo moyoni mwake matamanio na mategemeo
yasiyo kifani, sehemu yake moja ya milioni yasiyoweza kukidhika kwa njia ya
uwezo wake mwenyewe. Kwa hivyo mwishowe atabakia mpweke akiwa na matatizo na
mateso mazito. Kuiamini Kadari kumpunguzia mwanadamu uzito wa mizigo yote kwa
yenyewe kuuhimili uzito huo. Huipa roho raha na utulivu, na huiwezesha kupata
uhuru mkamilifu.
Kuiamini Kadari huinyang'anya
uhuru ileroho ya matamanio ya kimwili, na huvunja ile nguvu ya matamanio
yanayomshikilia huyo mwanadamu. Kuiamini Kadari humpa mtu raha na furaha kubwa
isiyoelezeka. Tutaonyesha hiyo furaha kwa mlinganisho ufuatao:
Fikiria watu wawili walioingia kwenye jumba la
mfalme. Mmoja wao hamtambui mfalme, na anajaribu kuishi kule kwa kujitwalia na
wizi.
Lakini anapata tabuna matatizo kama kulidhibiti
hilo jumba na wakazi wake, Kwa vile bustani huhitaji uangalkizi maalum, na
mambo ya jumbani humo Yanahitaji mahesabu na uangalizi sahihi kabisa. Kuendesha
mashine za mle, kuwalisha aina aina ya wanyama waishio humo kunampa taabu sana.
Kwa hivyo alitaabika sana, na peponi hapo pakageuka kuwa motoni kwake. Hatimaye
akafungwa kwa sababu ya dosari za uendeshaji na ufisadi wake.
Yule mwingine, alitambua mfalme,
na alielewa kuwa yeye ni mgeni wake.
Alihisi na aliamini kuwa mambo
yote ya jumba na bustani lile huendelezwa chini ya mamlaka na utawala wake. Alikuja kuelewa kuwa ni mfalme
mwenyewe ndiye anawajibika kikamilifu kulitawala jumba lile, kwa hivyo anafaidi
kuishi mle bila kuingilia kati jambo lolote. Akasahau mambo mengine aliyoyaona
hayamridhishi, akiiamini huruma ya mfalme na haki ya utawala wake, na hivyo
akaishi maisha mazuri ya kuridhika.
Fikiria mlinganisho huu na izingatie maana ya
usemi huu: “Anayeiamini Kadari huwa hana
wasiwasi”.
Maudhui ya
Nne
Imethibitishwa katika Maudhui ya
Kwanza kuwakila linaloamuliwa na Kadari ni zuri, na kuwa hata kama baadhi ya
matukio yaelekea ni maovu, kwa hakika ni mazuri; na mambo mabaya kwa yakini ni
mazuri Ikiwa hii itapingwa kwa kuhoji kuwa mbona maafa na mikosi anayoipata
mwanadamu inapingana na haya, jibu ni kama ifuatavyo:
Hata kama wewe, roho yangu yenye
matamanio ya kimwili na rafiki yangu, unaona mateso kwa sababu ya mahusiano
imara baina yako na kuwepo na upendo juu ya viumbe, basi kuwepo ni kuzuri kote
kwa vile huleta kila uzuri na ukamilifu. Ambapo kutokuwepo ni uovu kwa kuwa
dhambi zote na mikosi hutoka ndani yake. Kwa kuwa kutokuwepo ni kuovu, hali
zile ambazo zina dalili za kutokuwepo ndani yakezina sehemu fulani ya uovu. Kwa
hivyo maisha, nuru kali zaidi kuliko zote ya kuwepo, hukua kwa nguvu kadri
inavyozungukakatika hali tofauti. Husafishwa na hukamililishwa kwa njia ya
uzoefu wa matukio yanayojipinga, na huzaa matokeo yanayopendwa kwa kujivisha
ubora mbalimbali, na hivyo hushahidilia kwa udhihirisho wa Majina ya Kiungu. Ni
kwa sababu hii viumbe hai hupita katika hali nyingi, na hupata uzoefu wa
kuteswa kwa mikosina shida, kwa hiyo husafisha maisha yao. Katika kila moja ya
shida hizi, wao hujadidisha nuru ya kuwepo kwao, na huondoka kutoka kwenye giza
hasi la kutokuwepo.Kukaa bure, kukinai, kote huko - kiubora na kama hali ni
aina ya kutokuwepo. Hata raha kuu zaidi kuliko zote imeshushwa na kuwa si
lolote wala chochote kwa ajili ya kukinai .
Kwa ufupi: Kwa kuwa masiha huonyesha
udhihirisho wa Majina Mazuri ya Allah, kila kitu kinachotokea ndani yake ni
kizuri. Hebu tuchukue mfano wa mtu tajiri na stadi sanawa ubuniaji mitindo ya
nguo anamuajiri mtu wa kawaida kuonyesha kazi zake za sanaa kwa kulipwa
mshahara. Anamtaka mtu huyo avaenguo iliyopambwa na nakshi na vito ambayo
itaonyesha usanii wake na utajiri wake usio kifani. Analipamba hilo vazi juu ya
huyo mtu, na kulipa maumbo mbalimbali. Ili kuonyesha kila aina ya sanaa wake,
analika, analibadilisha, analirefusha na analifupisha. Itakuwa ajabu kiasi gani
basi iwapo huyo muajiriwa atasema: “Unanitaabisha. Unanifanya niiname na
nisimame.Huko kulikata na kulifupisha hili vazi ambako kunanifanya niwe mzuri
zaidi, wewe unauharibu uzuri wangu!” Je ana haki ya kumwambia, “Wewe
unanikatili na unanionea”?
Halikadhalika, Muumbaji huwavisha
viumbe hai vazi la kuwepo, lenye kutiwa vito vya hisia, sababu, akili, na moyo.
Anakata sanamu za vazi hilo ili kulipa maumbo mbalimbali, na Analiongezea
uzuri, na Anaonyesha uzuri wa Majina Yake Mazuri. Zile hali zinaonekana
kusababisha mikosi na uchungu kwa kweli ni mimuliko ya Hekima ya Kiunguambayo
inarudisha miale ya huruma na inao uzuri wa siri.
YAKUMALIZIA
[Hii ina ibara tano ambazo zina
maagizo ya ukweli ambao waasi roho asi na yenye majivuno na ya kimwili sharti
iyatii.]
Ibara ya
Kwanza
Kwa kuwa vitu vipo na
vimetengenezwa kwa ustadi, basi Mtengenezaji Mkuu sharti Awepo. Ikiwa kuwepo
kwa kila kitu kumetokana na na Mmoja tu tu, basi uumbaji wa vitu vyote ni rahisi
kama uumbajiwa kitu kimoja peke yake. Hii isingekuwa hivyo kama tungewafikiria
waumbaji wengine. Tunapokiri kuwa uumbaji wa a rdhi na mbingu ni kazi ya
Muumbaji mmoja tu, hatukosi kuamua kuwa Muumbaji Mwenye Hekima na Stadi
hangeruhusu mpangilio potofu utokee kwa kuwaruhusu wengine wavitawale viumbe
hai. Asingeishusha hadi iwe kichekesho Dhamira ya Kiungu kwa kuleta kuwepo kwa
viumbe vyote kwa kuruhusu pawa awe nayoyeyote ambaye siye Yeye Mwenyewe, na
wala hatoruhusu viumbe wamuabudu au wamshukuru mwingine yeyote.
Ibara ya
Pili
Ewe roho yangu ya majivuno na ya kimwili! Uko kama mdhabibu. Pawa nyingine, sio wewe.
Imekufanya wewe uvae kichala cha dhabibu kama vazi, na usijigambe.
Ibara ya
Tatu
Ewe roho ya maringo ya kimwili! Usijivunie
huduma zako katika dini Ya Allah. Kama ilivyosemwa katika mapokeo ya Mtume:
“Kwa hakika Allah Anaweza kuiimarisha dini hii piakwa njia ya mtu fisadi.”Wewe
sio nadhifu, kwa hiyo sharti ujihesabu wewemwenyewe kama mtu fisadi. Jivue kule
kujitamani mwenyewe na majivuno kwa kuhesabu huduma na ibada yako kama
shukurani mafao aliyokupa Allah zamani, na wajibu unaotarajiwa na utu wako, na
matokeo ya wewe kuwa kazi ya sanaa ya Allah.
Ibara ya
Nne
Ikiwa unataka kupata ujuzi wa
ukweli na hekima ya kweli, jaribu kupata ujuzi wa Allah na ujue kuwa uhalisi wa
uumbaji ina miale ya Majina ya Kiungu ya Ukweli na udhihirisho wa Majina na
Sifa Zake. Uhalisi
wa kila mwanadamu na wa kila kuwepo, kama kiroho au kimwili, kwa kukusudia au
utokukusudia, vyatokana na nuru ya moja ya Majina Yake.
Ewe roho yangu ya kimwili, ukijishikiza kwenye
maisha haya ya kiduni ya mpito, na unataka ukikimbie kifo, ujue kuw maisha ni
muda wa “sasa”, wakati u hai. Nyakati zote zilizopita, pamoja na vitu
vilivyokuwepo mle, vyote vimepita, na wakati ujao pamoja na yatakayotokana nao
havipo. Hii maana yake ni kuwa maisha yako ya kidunia ambayo unayategemea ni ya
muda mfupi; tena wanazuoni wengine wanaojua ukweli wanasema kuwa yana muda
mfupi tu. Watakatifu wengine wamefikia hata kuamua kuwa basi dunia haipo kwa
peke yake. Sasa, huu ndio uhalisi, kwa hivyo wachilia mbali maisha ya kidunia
na jaribu kuishi katika ngazi ya kiroho, na gundua jinsi maisha yanaweza kuwa
kamili.
Ingawa wakati uliopita na ujao vimekufa kwako
wewe, bado vi hai kwa watu wa kitakatifu amabao wanaishi maisha yao katika
nyanja ya kiroho. Kwa kuwa huu ndio halisi uliopo, toa machozi kwa moyo wako
wote, ewe roho yangu ya kimwili, na ulie kwa uchungu hivi:
Mimi ni wa kufa
lakini sivitaki vitu vya kufa.
Mimi sijiwezi
kwa lolote hivyo sivipendi vitu visivyojiweza kwa lolote.
Niliisalimisha
roho yangu kwa Mwenye Rehema Zote, hivyo sihitaji yeyote mwingine Namtaka
ambaye atabakia rafiki yangu daima.
Mie siye
ila punje isiyo maana, lakini nalitaka Jua la Milele.
Mie si kitu
kwa yakini ila ninaviombea viumbwaji vyote.
Ibara ya
Tano
Ibara hii ilinitokea kwa Kiarabu,
na ikaandikwa kwa Kiarabu. Hii ibara ya Kiarabu inaelezea moja ya maskani
thalathini na tau za kutafakari juu ya Allah ni Mkuu Zaidi kuliko wote (Allwaahu Akbar).
Allah ni
Mkuu zaidi kuliko wote: Yeye ni Mwingi (All-) wa Pawa, wa Hekima, Wa Ukarimu,
wa Huruma, wa Uzuri, ni Mwandishi wa Milele. Uhalisi wa
uumbajiwote na katika sehemu zake zote, una kurasa na karatasi. Nauhalisi wa
viumbe vile kwa ujumla na kwa kila kimoja, na katika kuwepo kwao na katika
kuendelea, si lolote ila:
*mistari
iliyochorwa na Kalamu ya Amri na Kadari ya Allah, na kuamuru na kutamalaki
Kwake kwa Kujua na kwa Hekima;
*Maandiko
ya kistadi yaliyoandikwa kwa kalamu za Hekima na Ujuzi Wake, na kuunda na
kudhibiti kwa sanaa na upendeleo;
*Kuremba
kwa 'mkono' unaong'aa kwa sanaa Yakena upendeleo, na kupamba na kumulika kwa
hisani na upaji.
*Maua ya
siri za Upendeleo na Upaji Wake, na kujulisha na kupendeka, kwa rehema na
mafao);
*Matunda ya
mmwaiko waRehema Yake na Mafao na Huruma na Upendo, kwa hisani na ukamilifu;
*Na
mimuliko namidhihirisho ya Hisani na Ukamilifu Wake, kama ilivyoshuhudiwa kwa
udhihirisho wa kudumu na mrudisho wa daima wa hisani bora sana ya milele kwenye
mchanganyiko wa viyoo (vya viumbe), na katika mlolongo wa vitu katika kupita
kwa majira, karne, miaka, na kwa utoaji wa milele wa mafaokwamuda wote wa
kupita kwa viumbe na siku na watu.
Naam, kazi
kamilifu huashiria, kimantiki, tendo kamilifu, na tendo kamilifu huashiria, kwa
njia ya kuelewa, jina kamilifu; na jina kamilifu huashiria bila shaka sifa
kamilifu. Sifa kamilifu sharti iashirie ubora kamilifu; na ubora kamilifu bila
shaka huashiria ukamilifu wa Asili, Wakala, yaani sahihi kwa hiyo Asili, Ambaye
ndiye Ukweli Mkuu.
Hakika
kudumu kwa muda mfupi kwa viyoo hivyo, ambamo udhihirisho huonyeshwa, na vifo
vya viumbe, pamoja na udhihirisho wa kudumu na mng'aro wa daima ni ushahidi wa
wazi kabisa kuwa huo uzuri wa bandia hautokani na viumbe vyenyewe; ni maelezo
timilifu na ushahidi dhahiri kabisa wa Uzuri wa kupita tu, na Utoaji usioisha
kujadidishwa wa Huyo Ambaye Lazima Yupo, Ambaye Ana MapenziYote wa Kudumu.
Ewe Allah!
Mmiminie Baraka bwana wetu Muhammad kutokea milele iliyopita hadi milele ijayo,
kwa vitu vyote ambavyoUjuzi wa Kiungu unajumlisha, na kwa familia yake na
Maswahaba, na wamiminie Amani.
KIAMBATANISHI
Kwa Jina la
Allah, Mwingi wa Rehema, na Huruma
[Kiambatanishi hiki kifupi kina umuhimu mkubwa
sana, na kina manufaa kwa kila mtu]
Kuna njia nyingi zinazoongoza kwa Allah
Mwenyezi. Njia zote hizi zinatokana na Qur'an, lakini zingine ni salama zaidi,
zinajumuisha mambo mengi zaidi na zinapelekeakwenye lengo moja kwa moja zaidi
kuliko zingine. Njiaambayo ilinifaa kutoka katika Qur'an kwa kutumia uelewaji
wangu mpungufu inategemea akili za kuona na kukiri kutoweza kujisaidia na ufukara mbele ya Nguvu na Utajiri wa Allah,
na inategemea upendo na kutafakari.
Akili za kuona za mwanadamu na kukiri
kutojiweza kwake ni njia ya hakika kama ilivyo njia ya upendo ya Allah, au hata
salama zaidi kuliko ile, kwa kuwa humkweza mwanadamu ili apendwe na Allah kwa
sababu ya kumuabudu kwa dhati Yeye. Akili ya kuona ya mwanadamu na kukiri
ufukara au upungufu wake hupelekea katika Jina la kiungu la Mwingi wa Rehema.
Upendounaathiri zaidi kuliko mapenzi, na hupelekea kwenye Jina la Mwingi wa
Huruma. Kutafakari kunang'aa zaidiNa kunafaa mambo mengi zaidi kuliko mapenzi
na hupelekea katika Jina la Mwingi wa Hekima .
Njia yetu hii sio sawa na madhehebu mengine ya
ya Kisufi ambayo yametunga hatua kumi za kutakasa na kuzinoa hisia kumi za nje
na za ndani za mwanadamu, na ambayo wafuasi wake hupendelea kuyasoma Majina ya
Allahbila kutoa sauti. Pia sio sawa na zingine ambazo zinafuata usomaji wa
hadharani na hutaka kumwezesha mtu kujitakasayeye mwenyewe pungufu zilizomo
ndani ya maskani saba za roho.
Njia yetu ina hatua nne, na badala ya kuwa tarika, ni Shari'a, au ukweli wenyewe (haqiyqah).
Misingi mikuu ya njia hii inategemea kufuata Sunna, kudumisha wajibu wa dini, kuepuka madhambi mabaya makuu, na
kudumisha sala tano vizuri, na kusoma maombolezi ya kumsifu Allah (tasbiyhat) baada ya kila sala.
Hatua ya kwanza ya njia hii imetajwa katika aya
ifuatayo ya Qur'an:
“53:32 Basi
msizitakase (msizisifu) nafsi zenu (na kujifanya hamna dhambi). Yeye Anamjua
sana aliyetakasika (na asiyetakasika).
[Falaa
tuzakkuw anfusakum huwa a'alamu bi manit-taqaa.]”
Hatua ya pili imetajwa katika aya ifuatayo:
“59:19Wala
msiwe kama wale waliomsahau Allah, na Allah Akawasahaulisha nao nafsi zao.[Wa laa takuwnuw kal-ladhiyna nasul-Lwaaha fa
ansaahum anfusahum.]”
Hatua ya tatu imeonyeshwa na aya ifuatayo:
“4:79Kila
wema uliokufikia umetoka kwa Allah; na kila ubaya uliokufikia unatoka nafsini
mwako. [Maa aswaabaka min hasanaatin
minal-Lwaahi, wa maa aswaabaka min sayyiaatin fa min-nafsika.]”
Hatua ya mwisho imeonyeshwa na
aya ifuatayo:
“28:88 Kila kitu kitakufa isipokuwa Sura Yake na ridhaa Yake.
[Kullu shay-in haalikun illaa Wajhahuw.]”
Yafuatayo ni maelezo machache ya
hatua hizi nne:
Hatua ya
kwanza: Mwanadamu kamwe asijihesabu kuwa asiyeweza kukosa wala kuwa hana dhambi,
kwa vile hujipenda yeye mwenyewe kwanza kwa sababu ya nafsi yake inayemtawala;
na kwa hivyo atajitolea mhanga kwa kitu chochote ili airidhishe. Hujisifu yeye
mwenyewe kama vile yu mungu, na anajifanya kuwa katakasika na kila upungufu au
dosari. Hujaribu kuthibitisha kuwa yeye hana hata hisia ya makosa na hujitetea
kwa nguvu sana kiasi kwamba utafikiri yeye kakithiri katika kujipenda mwenyewe.
Tena hutumia vipawa alivyopewa yeye vya kumsifia na kumshukuru Allah, kwa
kuisifia nafsi yake yeye mwenyewe, na hivyo huonyesha maana ya aya ifuatayo:
“25:43 Je umemuona yule aliyeyafanya matamanio yake kuwa mungu wake?
[Ara-ayta manit-takhadha ilaahahuw hawaa.]”
Hujisifu yeye mwenyewe,
hujitegemea yeye mwenyewe, na hujitamani yeye mwenyewe. Njia pekee ya mwanadamu
kujitakasa katika hatua hii ni kwa kujihesabu kuwa yeye ni anayeweza kukosa,
anayewajibika, na hata mwenye wepesi wa kupatwa na kosa.
Hatua ya
pili: Kama
hiyo aya ya:
“59:19Wala msiwe kama wale waliomsahau Allah, na Allah
Akawasahaulisha nao nafsi zao.” Inavyofundisha, mwanadamu husahau mwenyewe
wepesi mno, na hajijui. Kamwe hataki kukumbuka kifo, ingawa hupenda kuwahesabu
wengine kuwa ni watu wa kufa. Hurudi nyuma wakati wa kuvumilia taabu na kutoa
huduma, lakini hufikiri kuwa yeye ana haki ya kuwa wa kwanza kupokea zawadi
wakati wa kuvuna matunda unapowadia.
Mwanadamu naweza kujitakasa yeye
mwenyewe katika hatua hii kwa kutekeleza majukumu, na awe tayari kwa kifo, na
kwa kusahau zawadi yeyote anayoweza kuipata.
Hatua ya
tatu: Kama
aya hiyo ya:
“4:79Kila wema uliokufikia umetoka kwa Allah; na kila ubaya
uliokufikia unatoka nafsini mwako.” Inavyofundisha, ile nafsi inayoamrisha
maovu kila mara hujilimbikizia uzuri kwake na hujiona, ambapo kwa hakika
angeuona upungufu na ukosefu wake na atoe shukrani kwa Allah na amsifu Yeye kwa
jema lolote analoweza kulitenda. Kwa muujibu wa aya ifuatayo:
“91:9 Bila shaka amefaulu aliyeitakasa nafsi yake. [Qad aflaha man zakkaahaa.]”
Kutakasika kwake katika hatua hii
kunawezekana kwa yeye kujua ukamilifu wake katika kuongopa kuhusu kukiri kwake
kuwa sio mkamilifu, pawa yake ya kutambua kuwa hajiwezi kitu yeye mwenyewe, na
utajiri wake katika kukubali ufukara na upungufu wake.
Hatua ya
nne: Kama
inavyofundisha aya ifuatayo:
“28:88Kila kitu kitakufa isipokuwa Sura Yake na ridhaa Yake.”,
mwanadamu akitawaliwa na roho yake inayomwamrisha maovu, hujihesabu kuwa yupo
huru kabisa na anaishi kwa nguvu zake yeye mwenyewe. Tena hufikjia hata
kujidaia uungu yeye mwenyewe, na humuasi hata Mwuumba wake Ambaye Yeye peke
Yake Ndiye Anayestahili kuabudiwa. Anaweza kujiokoa kutoka katika hali hii ya
hatari kwa kuuona ukweli kwamba kila kitu kwa hakika hakipo kwa muujibu wake,
cha kubahatisha tu, cha kudumu muda mfupi tu, na cha kufa tu, lakini ni kwa
ajili tu ya kuwa kiyoo inachorudisha Majina ya Mtengenezaji Mtukufu, na
anawajibika katika kazi mbalimbali yeye amekuwepo, na anapata uzoefu.
Mwanadamu anaweza kujitakasa
katika hatua hii kwa kuona kuwa kuwepo kwake kunategemea kukiri kwake kuwa kwa
yakini hayupo. Sharti
ajue kuwa, akijihesabu kuwa yeye yupo kwa nguvu yake mwenyewe, anajitumbukiza
katika shimo jeusi kabisa la kutokuwepo. Kwa maneno mengine, iwapo anategemea
kuwepo kwa nguvu zake mwenyewe, ampuuze Mwumbaji Halisi, basi kuwepo kwake kwa
muda mfupi kama kwa kimetameta huzama kwenye giza kuu kabisa la kutokuwepo.
Endapo, kinyume chake, ataacha majivuno na kujifikiria mwenyewe, na atambue
kwamba yeye si chochote ila kiyoo ambamo Mwumbaji Halisi anajionyesha mwenyewe,
kisha hupata kuwepo kwa milele. Kwa hivyo, kwa sababu amemgundua Anayestahiki
,Ambaye kudhihirishwa kwa Majina Yake kwasababisha vitu vyote kuwepo,
huhesabika kuwa amepata kila kitu.
Ya Kumalizia
Njia hii ndio mbinu ya kupenda na kutafakari,
na ya mtukutambua udhaifu na upungufu wake yeye mwenyewe, na imeelezwa hapa nyuma
na katika MANENO yaliyopita, ambayo yanahusu ilmu ya ukweli na Sheria, na
uhekima wa Qur'an.
Njia hii inapelekea kwenye lengo wepesi zaidi,
kwa kuwa ndio rahisi zaidi na ya mioja kwa moja kuliko zote, na ina hatua nne
tu. Kutambua kwa mwanadamu kuwa hana uwezohumpelekea amtegemee Allah peke Yake,
mara atakapofaulu kujivua athari za nafsi yake inayomtawala. Upendo, ambao
unahesabika kuwa ndio njia ya haraka zaidi kuliko zote, unaweza kupelekea kwa
Mpendwa wa kweli pale tu inapotenganishwa na mpendwa wa bandia wa kudumu muda
mfupi.
Njia hii ni salama kuliko njia zingine, kwa
kuwa badala ya kumpelekea mtu kutamka maneno ya majivuno, na kutoa madai ya
uongo, inamlazimisha kutambua kutojiweza kwake, na kujisingizia yeye mwenyewe
dosari zake zote.
Njia hii ni “Njia kuu”, pana zaidi na ya dunia
nzima. Kwani, ili upate ufahamu wa saa zote wa kuwepo kwa Allah, haihitaji
kukanusha wala kupuuza kuwepo kwa ulimwengu, Kama inavyotakiwa na wale
wanaoitikadi Umoja wa Yeye [Wahdat
Al-Wujud], au Umoja wa Aliyeshahidiliwa Wahdat
al-Shuhud]. Badala yake inakiri kuwepo kwa ulimwengu kama ambavyo inasemwa
kwenye Qur'an, kwa kutambua kuwa inatokana moja kwa moja na Mwuumbaji Mtukufu.
Inahesabu vitu vyote kuwa ni viyoo ambamo udhihirisho wa Majina ya kiungu
hurudishwa, na haihesabu viumbe kuwa huwapo kwa nguvu zake vyenyewe wala
vinavyojiendeleza vyenyewe, bali inavihesabu kuwa ni udhihirisho wa Majina Yake
na hivyo vinashughulikia huduma Zake.Inamuepusha mwanadamu asiwe asiyejali na
daima ajuekuwapo kwa Allah kwa kufungua njia ya kufika Kwakekupitia kila kitu.
Kwa ufupi: Njia hii inavihesabu viumbe
kuwa havipo wala havifanyi kazi kwa niaba yake vyenyewe Lakini viumbe hufanya
kazi, kwa muujibu wa njia hii, kama alama na maafisa wa Allah, Mwenyezi..
* * *